Header Ads Widget

MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA MAHAKAMA KUU,RC KHERI APONGEZA MAHAKAMA

Na Matukio Daima Media Iringa 

 Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James, ameipongeza Mahakama Kuu Kanda ya Iringa kwa kutimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005, akisisitiza kuwa chombo hicho kimeleta mageuzi makubwa katika utoaji haki na kukuza imani ya wananchi kwa mfumo wa mahakama nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo  James alisema maadhimisho hayo yanayofanyika chini ya kaulimbiu “Safari ya Miaka Ishirini ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Iringa” ni ushahidi wa safari yenye mafanikio ambayo yamechangia maendeleo ya Mkoa wa Iringa na Taifa kwa ujumla.

Alibainisha kuwa tangu kuanzishwa kwa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, kumekuwa na maboresho makubwa ikiwemo.

Kuongezeka kwa miundombinu ya majengo ya Mahakama kuwa uongezekaji wa Majaji na watumishi,Matumizi ya TEHAMA katika uendeshaji wa mashauri,Kuimarika kwa imani ya wananchi kwa mfumo wa utoaji haki.


Alisema kuwa kuanzishwa kwa kanda hiyo kulilenga kupunguza mlundikano wa mashauri kwenye kanda nyingine na kurahisisha upatikanaji wa huduma za mahakama kwa wakazi wa Iringa, Njombe na maeneo ya jirani.

Aidha alisema kuwa kumekuwepo  ushirikiano Imara Kati ya Serikali na Mahakama.

 James alisema  kuwa Serikali imeendelea kuuthamini na kuimarisha ushirikiano wake na Mahakama kama mhimili muhimu wa dola  na kutaja maeneo ambayo Serikali imekuwa ikishirikiana na Mahakama kuwa ni pamoja na Kuboresha usalama wa majengo,Kutoa maeneo kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama za Mwanzo,Kusaidia elimu kwa wananchi kuhusu masuala ya sheria pamoja na Kushirikiana katika mapambano dhidi ya rushwa.



“Serikali na Mahakama zikifanya kazi kwa kuheshimiana, wananchi hunufaika,” alisema RC.

Akitaja mchango wa Mahakama katika maendeleo, Mkuu wa Mkoa alisema uwepo wa Mahakama Kuu umeongeza imani ya wawekezaji, kuboresha ufanisi wa mashauri ya ardhi, biashara na jinai, pamoja na kupunguza migogoro ya kijamii.

“Maendeleo ya kiuchumi hayawezekani bila amani na utawala bora. Mahakama ndiyo injini inayolinda misingi hiyo,” aliongeza.

Alisema kuwa katika kuelekea kilele cha maadhimisho tarehe 15 Desemba 2025, shughuli mbalimbali zimepangwa kufanyika  kama 8–12 Desemba 2025 kutoa  Elimu kwa umma kupitia redio na televisheni kuhusu huduma za mahakama, mirathi, uandishi wa wosia, usuluhishi (ADR), utatuzi wa migogoro, haki za watoto, ndoa na talaka, na matumizi ya TEHAMA katika mashauri.

Pia mkuu huyo wa mkoa alisema 12 Desemba 2025 (Saa 2:00–5:00 asubuhi) Mdahalo utakaofanyika katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki Ruaha (RUCU) huku 13 Desemba 2025 (Saa 12:30–3:00 asubuhi)Matembezi ya Maadhimisho na kufungwa kwa wiki ya elimu kwa umma.


Wakati 15 Desemba 2025 ni Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 20 ya Mahakama Kuu Kanda ya Iringa kuwa anawakumbusha watumishi wa Mahakama na wadau wote wa haki jinai na madai kuendeleza na kuishi kaulimbiu ya Mahakama ya Tanzania.

"Wananchi wanaombwa kutambua kwamba haki inapopatikana kwa wakati, jamii hujenga imani, na unapojengeka msingi wa imani, uchumi na ustawi wa jamii huzidi kukua Tutumie ipasavyo fursa ya maadhimisho haya kujifunza zaidi kuhusu mfumo wa utoaji haki"


"Pia Tushiriki shughuli zote zilizo wazi kwa umma ili kuongeza uelewa na ukaribu kati ya wananchi na Mahakama na Tuendelee kushirikiana na Mahakama pamoja na Serikali katika kulinda amani, uadilifu na utulivu wa jamii "alisema Rc Kheli


kuwa kama mkoa unatambua jitihada kuwa zinazofanywa na mahakama kuu hivyo wanaendelea kupongeza sana .

"Natoa pongezi za dhati kwa Mheshimiwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa na timu yake kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuhakikisha haki inapatikana kwa wakati Pia nawashukuru nyinyi waandishi wa habari kwa mchango wenu muhimu katika kuelimisha jamii kuhusu masuala ya sheria, haki na utawala bora.

Alisema kuwa Maadhimisho hayo  ya miaka 20 si tukio la kawaida, bali ni alama ya maendeleo, ustahimilivu na utumishi uliotukuka. Ni hatua muhimu tunayopiga kama Taifa katika kuimarisha mifumo ya utoaji haki.

PAKUA APP YA MATUKIO DAIMA BURE BOFYA LINK HII

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI