Header Ads Widget

MBUNGE VILLA AWATAKA MADIWANI MAFINGA KUWAJIBIKA VEMA KWA WANANCHI

 


NA MATUKIO DAIMA MEDIA.

MBUNGE jimbo la Mafinga mjini Dickson Lutevele Villa amewataka Madiwani wa halmashauri ya Mji wa Mfinga kwenda kufanya kazi ya kuwatumikia vema wananchi. 

Villa amesema hayo leo wakati wa kikao cha baraza la madiwani ambapo baada ya kuapishwa walimchagua kwa kura zote za ndio aliyekuwa mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kipindi kilichopita Reginand Kivinge kuendelea kuongoza tena Halmashauri hiyo. 

Uchaguzi huo uliofanyika  baada ya madiwani hao kuapishwa rasmi na Hakimu  Mkazi wa wilaya ya Mufindi Edward Uphoro kuwa madiwani baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29 mwaka huu. 


Katika uchaguzi huo Kivinge alikuwa mgombea pekee aliyegombea nafasi ya kiti huku Steven Msigwa akiwa mgombea pekee nafasi ya umakamu mwenyekiti ambapo wote wawili wameshinda kwa kura zote za ndio 12 zilizopitwa. 

Msimamizi wa uchaguzi huo katibu tawala wa wilaya ya Mufindi Reuben Chongolo aliwashukuru wajumbe hao kwa kukamilisha zoezi hilo kwa umakini mkubwa. 

Akizungumza na matukio Daima Media Lutevele alisema kuwa mara baada ya kuapapishwa tayari amefanya ziara katika jimbo lake kw kuwafikia makundi maalumu kama vile idara za serikali za mafinga mji,

"Nimefanya vikao na makundi ya ma afisa usafirishaji kwa maana ya boda boda,tayari nimetembelea kata sita bado kata tatu amabzo kulingana na kikao hiki nimekatish ila nitamalizia"


Lutevele alisema kuwa amewasikiliza vijana ili kujua changamoto zao na kutamani kusikia ni nini wanataka serikali iwafanyie ili atakapoingia katika viko vya bunge aweze kuwasemea mipango yao ili iweze kutimizwa.

"Nampongeza Rais kwa kuona kuwa kuna haja ya kuunda wizara ya vijana,ikumbukwe tuna vijana wengi mtaana ambao wamejiajiri na kuajiri wengine kupataikana kwa hii wizara ya vijana itasaidia kuwasikiliza kwa ukaribu zaidi n kutatua changamoto zao"alisema

Akitoa salamu za wilaya katika baraza hilo la madiwani mkuu wa wilaya ya Mufindi DKT Linda Selekwa mbali ya kuwapongeza madiwani hao kwa ushindi bado aliwataka kwenda kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi ili wananchi wanufaike na utendaji wao badala ya kwenda kuonesha ujuaji na mivutano isiyo na taji kati yao na watendaji. 

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI