Na. Matukio Daima Media, Dar es salaam.
KAMPUNI ya 361 Degrees Africa leo Desemba 3, 2025imezindua rasmi Miss World Tanzania, jukwaa la kitaifa linalolenga kutambua, kulea na kuwawezesha wasichana wa Kitanzania ili kuwakilisha Taifa kwa heshima, urembo, akili na dhamira.
Tukio la uzinduzi huo limefanywa na Kaimu Katibu Mtendaji, Bw. Edward Buganga ambao ulienda kwa kuonesha makala (Documentary) maalum ya historia ya Warembo wa Tanzania waliweza kuwa alama katika mashindano hayo hapa nchini.
Awali, akizungumza wakati wa Uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Kitaifa wa Miss World Tanzania, Mustafa Hassanali amesema, Uzinduzi huo unaashiria mwanzo wa kipindi kipya chenye mwelekeo mpya na wa kisasa kwa shindano hilo lenye hadhi kubwa.
"Miss World Tanzania inalenga kuwatambua na kuwalea wanawake vijana wenye uwezo wa kipekee wanaoonyesha umahiri, uongozi na falsafa ya kimataifa ya Miss World ya “Beauty with a Purpose.
“Miss World Tanzania si shindano tu; ni fursa ya kubadilisha maisha ya vijana wa kike Nchini.
Dhamira yetu ni kutoa jukwaa linalokuza sauti zao, kuimarisha jamii zao na kuwaandaa kuiwakilisha Tanzania kwa fahari na ubora katika jukwaa la kimataifa la Miss World.”
Ili kuhakikisha ushiriki wa Nchi nzima, mashindano ya ngazi ya mikoa yatafanyika kupitia wamiliki wa leseni wa Miss World Tanzania watakaorasimishwa Nchini kote.
"Matukio haya yatachagua washiriki bora ambao watapanda hatua hadi fainali za Kitaifa jijini Dar es Salaam, hivyo kuhakikisha ujumuishwaji na fursa sawa kwa wasichana kutoka kila mkoa.
361 Degrees Africa inawaalika watu binafsi, taasisi na waandaaji wa matukio wanaotaka kuandaa mashindano rasmi ya Miss World Tanzania ngazi ya Mkoa kuwasilisha maombi ya kupata haki za leseni.
Wamiliki watakaopitishwa watapewa mamlaka ya kipekee katika maeneo yao husika. Mshindi wa shindano la kitaifa atabeba taji la Miss World Tanzania na kuiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika shindano la Miss World 2026 kama Balozi wa urembo, utamaduni na dhamira ya ubinadamu.
"Umma unahimizwa kufuatilia safari hii kupitia majukwaa rasmi ya kidigitali ya Miss World Tanzania pamoja na matukio yajayo ya kitaifa katika (missworldtanzania)" Amesema Mustafa Hassanali.

.jpg)








0 Comments