Header Ads Widget

MAYALA AAHIDI KUSIMAMIA MAENDELEO BARIADI VIJIJINI.

 

DIWANI Mteule wa Kata ya Kasoli wilayani Bariadi Mkoani Simiyu kupitia CCM, Lucas Mayala.


Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.


DIWANI Mteule wa Kata ya Kasoli wilayani Bariadi Mkoani Simiyu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Lucas Mayala amesema kuwa atahakikisha anasimamia Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya wilaya ya Bariadi na kwamba hatovumilia watumishi wazembe pamoja na wakandarasi wanaokwamisha shughuli za serikali.



Amesema kuwa Wajibu wa serikali ni kuwatumikia wananchi na wao viongozi wanawajibika kusimamia miradi ya Maendeleo inayoletwa na serikali ili kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi bila ubaguzi wowote. 


Akizungumza leo mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mayala amesema kuwa atahakikisha anaisimamia Halmashauri ili kutekeleza Ilani ya CCM na kwamba watashirikiana na Madiwani wenzake kufungua na kuimarisha Barabara ili kurahisisha shughuli za Uchumi, usafiri na usafirishaji. 


"Tutaendelea kuimarisha sekta za Elimu na Afya kwa kuboresha madarasa, zahanati na nyumba za watumishi.. tuna Madiwani wapya 16 ambao tutakuwa na kasi ya Utekelezaji wa miradi ya Maendeleo, lengo ni kuboresha huduma za Wananchi, nitawatumia kama chachu ya Maendeleo hasa kusimamia fedha za mikopo ya vijana, Wanawake na walemavu " amesema. 


Amesema kuwa kipaumbele cha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha ustawi wa Maendeleo ya wananchi huku akiwasisitiza watendaji na wakandarasi kwamba hawatovumiliana na badala yake watembee kwa Kasi ili kusimamia na kutekeleza miradi ya Maendeleo kwa usawa unaotakiwa. 


Uchaguzi wa kumpata Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri kupitia CCM, umekamilika ambapo Mayala amepata kura 19 dhidi ya mshindani wake Isack Masunga aliyepata kura 9, hivyo Mayala atapigiwa kura kwenye Baraza la Madiwani baada ya kuwa amekula kiapo cha kuwa Diwani.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI