Na Fadhili Abdallah,Kigoma
MBUNGE wa jimbo la Kigoma Kaskazini Halmashauri ya wilaya Kigoma mkoani Kigoma Kiza Mayeye amesema kuwa amedhamiria kuwa sauti ya wananchi wa jimbo hilo katika kuwasemea na kutetea changamoto zao atakazozipeleka kwenye bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba hatakuwa bubu.
Mayeye alisema hayo akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Tarafa Kijiji cha Mwandiga Halmashauri ya wilaya Kigoma ambapo alisema kuwa baada ya kuwa mbunge wa jimbo hilo amedhamiria kwa dhati ya moyo wake kushirikiana na watu wote kuhakikisha wanaleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo hilo.
Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Tarafa kijiji cha Mwandiga Halmashauri ya wilaya Kigoma mkoani Kigoma
Kutokana na hilo Mbunge huyo alisema kuwa uwepo wa Amani na usalama ndiyo njia pekee ambayo itamuwezesha kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kwa ufanisi hivyo amewataka wananchi wa jimbo hilo kumpelekea mawazo yao na mipango ambayo anataka wafanye pamoja ili kuhakikisha mipango ya maendeleo inatekelezwa kwa haraka.
Akieleza vipaumbele vyake alisema kuwa moja ya jambo kubwa ambalo amepanga kuanza nalo kwa sasa ni elimu ambapo anakusudia kumaliza tatizo la upungufu wa madawati ili kuondoa changamoto ya wanafunzi kukaa chini.
Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha ACT Wazalendo mkoa Kigoma Ibrahim Sendwe akizungumza katika mkutano wa hadhara wa mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini Kiza Mayeye uliofanyika uwanja wa tarafa kijiji cha Mwandiga mkoani Kigoma
Alisema kuwa kwa sasa yeye ni mbunge wa wananchi wote bila kuwa na ubaguzi kwa chama chochote na hivyo amewaomba wananchi wa jimbo hilo kukutana naye na kumpa mawazo na mipango yao kwa ajili ya kuleta maendeleo kwenye jimbo hilo sambamba na kuangazia uboreshaji wa barabara kuu na barabara za mitaani ili kuhakikisha zinaptika wakati wote.
Awali Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha ACT mkoa Kigoma, Ibrahim Swende amewataka wananchi wa jimbo la Kigoma Kaskazini kuondoa mawazo kuwa mbunge huyo ni wa chama badala yake kila mmoja amuone kuwa ni mbunge wake na kushirikiana naye katika kuleta maendeleo.









0 Comments