MADIWANI wa Halmashauri ya Mji Mafinga mkoani Iringa wamemchagua kwa kura zote za ndio aliyekuwa mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kipindi kilichopita Reginand Kivinge kuendelea kuongoza tena Halmashauri hiyo.
Uchaguzi huo uliofanyika leo baada ya madiwani hao kuapishwa rasmi na Hakimu Mkazi wa wilaya ya Mufindi Edward Uphoro kuwa madiwani baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29 mwaka huu.
Katika uchaguzi huo Kivinge alikuwa mgombea pekee aliyegombea nafasi ya kiti huku Steven Msigwa akiwa mgombea pekee nafasi ya umakamu mwenyekiti ambapo wote wawili wameshinda kwa kura zote za ndio 12 zilizopitwa.
Msimamizi wa uchaguzi huo katibu tawala wa wilaya ya Mufindi Reuben Chongolo aliwashukuru wajumbe hao kwa kukamilisha zoezi hilo kwa umakini mkubwa.
Akitoa salamu za wilaya katika baraza hilo la madiwani mkuu wa wilaya ya Mufindi DKT Linda Selekwa mbali ya kuwapongeza madiwani hao kwa ushindi bado aliwataka kwenda kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi ili wananchi wanufaike na utendaji wao badala ya kwenda kuonesha ujuaji na mivutano isiyo na taji kati yao na watendaji.
Huku mbunge wa Mafinga mjini Dickson Lutewele Villa akiwapongeza madiwani wote kwa kuapishwa na kuwaomba kwenda kufanya kazi ya kuwatumikia vema wananchi.

















































































































































0 Comments