Kikosi cha Kombaini ya Makamba kutoka mkoa Burunga nchini Burundi ambacho kitacheza fainali na Kigoma Ujiji katika mashindano ya ujirani mwema yanayofanyika nchini Burundi
Na Fadhili Abdallah,Burunga Burundi
Timu ya Kombaini ya Makamba ya nchini Burundi na Timu ya Kombaini ya Manispaa ya Kigoma Ujiji ya mkoa Kigoma nchini Tanzania zinatarajia kumenyana katika mchezo wa fainali ya mashindano ya ujirani mwema baina ya timu za mikoa ya Burundi na kombaini za wilaya za mkoa Kigoma.
Timu ya Kombaini ya Makamba ya nchini Burundi ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuingia fainali baada ya kuifunga timu ya mkoa Ruyigi katika mchezo wa nusu fainali uliocheza jana kwa kufunga goli 2-1 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa mpira wa Nkurunzinza Peace Park Complex wilaya ya Makamba mkoa Burunga nchini Burundi.
Magoli ya Kombaini ya Makamba yalifunga na Niyomwungere Claude dakika ya 26 ya mchezo na goli la pili lilifungwa na Ntakirutimana Jules dakika ya 40 ya mchezo wakati goli la Ruyigi lilifunga na Fabric Nitunga dakika ya 71 ya mchezo.
Kombaini ya kikosi cha Manispaa ya Kigoma Ujiji ambacho kimeingia fainali ya mashindano ya ujirani mwema yanayofanyika wilaya Makamba mkoa Burunga nchini Burundi
Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini kutoka wizara ya Michezo,Sanaa na utamaduni Yussuph Singo (wa pili kulia) akikagua timu ya Kombaini ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kabla ya kuanza mchezo wa nusu fainali baina ya timu hiyo na Kombaini Ya Buhigwe zote za Tanzania katika mashindano ya ujirani mwema baina ya Tanzania na Burundi yanayofanyika mkoa wa Burunga nchini Burundi, Kigoma Ujiji itacheza fainali na Kombaini ya Makamba ya nchini Burundii Picha na Fadhili Abdallah
Kwa upande wake Kombaini ya Manispaa ya Kigoma Ujiji imeweza kuingia fainali baada ya mchezo wa nusu fainali kuifunga Kombaini ya wilaya ya Buhigwe kwa magoli 3-2 katika mchezo wa kusisimua ambao ulikuwa na mshindani mkubwa wakato wote wa mchezo kila timu ikitaka kucheza fainali.
Magoli ya Manispaa ya Kigoma Ujiji yalifungwa na mshambuliaji wake hatari Maneno Saidi katika dakika ya 27, dakika ya 44 na dakika ya 62 ya mchezo ambapo magoli ya Buhigwe yalifungwa na Zanzari Yekonia dakika ya 36 na dakika ya 55 ya mchezo huo.
Aidha kipindi cha pili Mchezo wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Ibrahim Amani alipata kadi nyekundu baada ya kumchezea madhambi mchezaji wa Buhigwe ndani ya eneo la 18 na hivyo Buhigwe kupata penati ambayo hata hivyo mpigaji wa penati hiyo Imani Gerson alikosa baada ya mpira kugonga mwamba na kurudi uwanjani ambapo uliokolewa na wachezaji wa Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro, wakuu wa wilaya za mkoa Kigoma, wakurugenzi na viongozi mbalimbali wa mkoa Kigoma wanatarajia kuhudhuria mechi hiyo ya Fainali nchini Burundi huku wakuu wa mikoa mbalimbali ya Burundi na viongozi waandamizi wa nchi hiyo wakitarajia kushuhudia fainali hizo.
Mwisho.








0 Comments