Kamati ya Madiwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Moshi Vijijini, imempitisha Diwani wa Kata ya Njiapanda, John Meela kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi kwa kupata kura 34 kati ya kura 45 zilizopigwa.
Akitangaza matokeo hayo, katibu wa CCM Wilaya ya Moshi vijijini, Ramadhan Mahanyu alisema katika uchaguzi huo, Meela alikuwa akigombea na Diwani wa Kahe Mashariki Kulwa Mmbando aliyepata kura 10 na Filbert Shayo wa kata ya Marangu Magharibi aliyepata kura moja.
Kwa upande wa makamu mwenyekiti, Mahanyu amemtangaza Diwani wa Mwika Kaskazi Samuel Shao kuchaguliwa kugombea nafasi hiyo kwa kupata kura 33 akiwashinda diwani wa Kirua Vunjo kusini aliyepata kura saba na diwani wa Kibosho kati kura tano.







0 Comments