Header Ads Widget

Dkt.MWIGULU KUWEKA JIWE LA MSINGI KAMPASI YA UDSM - LINDI

 

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinawaarifu wananchi kuwa Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la Kampasi ya UDSM–Lindi, itakayofanyika Ngongo, Manispaa ya Lindi, siku ya Jumamosi, 20 Desemba 2025, kuanzia saa nne asubuhi.

Mradi huu wa thamani ya Shilingi Bilioni 14.8 unatekelezwa kwa mkopo wa masharti nafuu wa Benki ya Dunia (HEET) na unajumuisha majengo ya utawala na taaluma, madarasa, maabara, karakana ya kilimo, mabweni ya wanafunzi pamoja na Kituo cha Utafiti cha Ruangwa. Utekelezaji umefikia asilimia 60.

Kampasi ya UDSM–Lindi inalenga kusogeza elimu ya juu karibu na wananchi na kuchochea maendeleo kupitia kilimo, ufugaji, nyuki na teknolojia ya chakula.

Wananchi na wadau wote mnakaribishwa kushiriki tukio hili la kihistoria.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI