Na COSTANTINE MATHIAS, Meatu.
MADIWANI wa Halmashauri ya wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, wamemchagua Anthony Philipo kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo baada ya kupata kura za ndio 41.
Philipo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Makao, amechaguliwa kwa kura 41 za ndio na Madiwani hao kushika nafasi hiyo kwa awamu ya pili baada ya kumaliza awamu ya kwanza 2020/2025.
Akizungumza mara baada kuchaguliwa, Philipo amewataka Madiwani kushirikiana huku akiwasisitiza watendaji wa serikali kufanya kazi kwa weledi.
"Tutafanya kazi Kwa weledi, Watendaji wanahitaji kuelekezwa, kushauriwa na kusaidiwa..Tukasimamie matatizo ya wananchi na nyie Wabunge mkatusemee serikali Kuu." Amesema.
Masunga Mizingo amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Kwa kupata kura 41 za ndio.
Katika Baraza hilo, Madiwani hao walikuwa viapo pamoja na kusaiini hati za viapo na maadili ya Utumishi wa Umma.
Mwisho.














0 Comments