Header Ads Widget

UTALII TANZANIA WAZIDI KUNOGA, MAWAKALA 120 WA MAREKANI WAVUTIWA



Mawakala wa utalii 120 kutoka nchini Marekani wameonyesha kuvutiwa na vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini Tanzania, hususan mandhari ya kuvutia, wanyamapori, na urithi wa utamaduni wa kipekee.

Tukio hilo limejidhihirisha katika usiku wa Novemba 7, 2025 kwenye hafla ya chakula cha usiku iliyofanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Mkoani Mara, iliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ajili ya kuwakaribisha mawakala hao waliowasili nchini kwa ziara ya kutembelea vivutio vya utalii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Excellent Guide Tours and Safaris,  Justin Alfred, amesema; "Tumevutiwa sana na mandhari ya Tanzania, hasa wanyamapori kama tembo, twiga, simba na nyati. Nchi hii ni salama, wananchi wake ni wakarimu, watalii wasisite kuja kuitembelea." 


Amesema lengo la ziara hiyo ni kuhakikisha Tanzania inatambulika zaidi duniani kama kitovu cha utalii barani Afrika kutokana na urithi wake wa asili, utamaduni na vivutio vya kipekee.

Kwa upande wake, Patricia Walker kutoka kampuni ya Nexion Travel ya Marekani, amesema kutembelea Tanzania ilikuwa ndoto yake tangu akiwa na umri wa miaka mitano, hususan kuona Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Naye, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Stephano Msumi, amewashukuru mawakala hao kwa kuichagua Tanzania kama sehemu ya kujionea vivutio vya asili, na kuwahimiza wawe mabalozi wazuri wa utalii watakaporejea nchini kwao.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI