Na Hamida Ramadhan, MatukioDaima Media Dodoma
MBUNGE wa Jimbo la Same Mashariki Mkoani Kilimanjaro Mhe. Anne Kilango Malecela amesema Rais Samia Suluhu Hassan amegusa mioyo ya Watanzania wengi kutokana na kumteua Mbunge wa Iramba Magharibi Mkoani Singida Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.
"Sifa kubwa ya Dkt. Mwigulu ni mtu anayefikika na lazima niseme ukweli kuna watu wakiwa mawaziri wanakuwa vigumu kuwafikia lakini kwa Mwigulu tangu akiwa Naibu Waziri, Waziri mpaka Waziri wa fedha ni mtu anayefikika na kila mtu na nyumbani kwake ni nyumbani kwa watu wengi." Amesema Mhe. Anna Malecela.
Amemuelezea pia kama mtu mwenye upendo kwa kila mmoja, akisema Wabunge wa Bunge la 13 pamoja na Wananchi wa Tanzania wamempata Kiongozi sahihi anayeweza kusimama kuwasemea na kuwatetea.
Malecela ametoa kauli hiyo mapema leo Novemba 13, 2025 Bungeni Mjini Dodoma wakati Rais Samia Suluhu Hassan alipowasilisha Jina la Dkt. Mwigulu Bungeni hapo ili kuweza kuidhinishwa kuwa Waziri Mkuu, akitarajiwa kuapishwa kesho Ijumaa Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tayari kuanza majukumu yake mapya kwa miaka mitano ijayo katika serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.






0 Comments