Wito umetolewa kwa kuilinda na kuitetea sifa ya Tanzania kuwa kisiwa cha amani, raha na furaha, Vijana wakitakiwa kujitenga na makundi na vishawishi vya kujiingiza kwenye vitendo vya kuhatarisha amani na mshikamano uliopo nchini Tanzania.
Akizungumza na Chombo hiki cha habari, Bw. Hussein Thomas Mawanga, amewataka pia Vijana kujifunza kutoka kwa nchi jirani, namna ambavyo ukosefu wa amani umewagharimu wengi, ukidhorotesha ustawi wa wananchi, kufifisha maendeleo ya Mataifa husika pamoja na kuharibu miundombinu mbalimbali na kusababisha maafa mengine ya kijamii, kiuchumi na kiusalama.
Bw. Mawanga amewasihi Vijana na Watanzania kwa ujumla kujifunza na kutambua umuhimu wa amani kwa maendeleo yao na ya Taifa kwa ujumla, akisema mpaka hii leo haamini kile kilichotokea Oktoba 29, 2025 na kusisitiza kila Mtanzania kutambua kuwa anao wajibu wa kulinda na kuitetea amani iliyopo nchini Tanzania





0 Comments