Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Tundu Lissu iliyopangwa kuendelea leo, Jumatatu Novemba 10.2025 imehairishwa hadi Jumatano ya Novemba 12 itakapotajwa tena Mahakamani hapo
Kesi hiyo ilipangwa kuendelea leo ambapo wa Jamhuri ilitakiwa kumleta Mahakamani hapo shahidi wa Nne (4), lakini kutokana na kile kilichoelezwa kuwa hali ya Jiji la Dar es Salaam kutokuwa kwenye utulivu mashahidi wa Jamhuri kutoka mikoa ya Ruvuma na Mbeya wameshindwa kusafiri kuja Dar es Salaam
Aidha, upande wa Jamhuri uliendelea kuieleza Mahakama kuwa kwa mantiki hiyo tarehe ya leo haukuwa umepata shahidi kwaajili ya kuendelea na kesi leo, na hiyo inatokana na sababu iliyoelezwa hapo awali ya kwamba Jiji la Dar es Salaam kutokuwa shwari kwa asilimia 100
Katika maelezo yake Wakili wa Serikali Mkuu Thawabu Issa ameiomba Mahakama kuhairisha kesi hiyo chini ya kifungu cha 302(a) cha Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai, Sura ya 20 (Toleo la 2023) kwa sababu ya kutokuwepo kwa mashahidi wameshindwa kusafiri kwa sababu za kiusalama
Upande wa Jamhuri uliiomba Mahakama kuhairisha kesi hiyo kwa siku 14, lakini katika maamuzi yake Mahakama kupitia Jaji Danstan Ndunguru ikatoa maelekezo kuwa shauri hilo linaahirishwa hadi Jumatano na si kwa siku 14 kama ilivyoombwa na Jamhuri





0 Comments