Na,Jusline Marco;Arusha
Maafisa 72 kutoka nchi za Tanzania ,Kenya, Uganda, Zimbabwe, Afrika Kusini, Malawi pamoja na Bangladesh wakiongizwa na Balozi Meja Jenerali Wilbart Ibuge mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi, wameanza ziara yao hii Leo jijini Arusha ya mafunzo katika Chuo hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha CPA Amos Makalla amewakaribisha Wakuu hao wa Vyombo vya ulinzi na usalama na Maafisa kutoka nchi 16 za Afrika na nje ya Afrika ambapo amewahakikishia usalama na utulivu kwa kipindi chote cha siku tano watakachokuwa kwenye mafunzo Mkoani humo.
CPA Makalla ametoa kauli hiyo leo wakati alipokuwa akiwakaribisha Maafisa hao ambapo amesema Mkoa wa Arusha ni Kituo cha Utalii kwa Kanda ya Kaskazini huku alisema kuwa, Arusha inaendelea vyema katika sekta ya utalii na sekta nyinginezo za kiuchumi na imeendelea kuwa salama na tulivu kutokana na ushirikiano mkubwa uliopo kati ya wananchi na Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.
Katika Programu hiyo ya mafunzo maarufu kama "Tentative Programme for Economy in Tourism", Washiriki hao wanatarajiwa kutembelea maeneo ya utalii ikiwemo Makao Makuu ya TANAPA, Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na kutembelea maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha kwa lengo la kujifunza tamaduni na mazingira mbalimbali ya Jiji hilo muhimu kwa uchumi, Utalii na shughuli nyingine za Kidiplomasia.





0 Comments