RAIS Dkt Samia Suluhu Hassan ameunda Tume Huru ya Uchunguzi kuhusu matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025. Mwenyekiti wa tume hiyo ni Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman.Rais Samia amesema lengo la kuundwa kwa tume hiyo ni kuhakikisha uwazi na uwajibikaji na kwamba matokeo ya uchunguzi yatasaidia kujenga imani ya wananchi na jumuiya ya kimataifa.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka Ikulu, wajumbe wengine walioteuliwa ni:
Profesa Ibrahim Khamis Juma - Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania
Balozi Ombeni Yohana Sefue - Mwanadiplomasia na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu
Balozi Radhia Msuya - Mwanadiplomasia na Balozi Mstaafu
Luteni Jenerali Paul Meela - Mwanadiplomasia na Balozi Mstaafu
Said Ally Mwema - Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Mstaafu
Balozi David Kapya - Mwanadiplomasia na Balozi Mstaafu
Dkt. Stergomena Lawrence Tax - Aliyewahi kuwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)






0 Comments