Header Ads Widget

PALIPO NA UTULIVU NA AMANI PANA MAENDELEO- HOKORORO

Na Matukio Daima Media

WANANCHI wa Kibaha Mkoani Pwani wamehimizwa kutunza amani katika maeneo yao ili waweze kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii hivyo kuwezesha ustawi na maendeleo yao na ya nchi kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Mkaguzi wa Polisi, Elieza Hokororo kutoka Kitengo cha Polisi Jamii Mkoa wa Pwani alipokua akizungumza na maafisa usafirishaji kwa njia ya Pikipiki maarufu kama Bodaboda, bajaji na wafanyabiashara wa kituo cha Mabasi Kibaha kuhusu ulinzi na usalama katika maeneo yao.


Mkaguzi Hokororo amewaeleza wafanyabiashara hao kuwa inapokosekana amani, wao kama maafisa usafirishaji hawawezi kutoka kufanya kazi za kupakia abiria au mizigo kutoka sehemu moja kwenda nyingine, hawawezi kupata chakula wala matibabu na huduma nyingine muhimu za kijamii.

Naye Msemaji wa wafanyabiashara wa kituo cha mabasi Kibaha, Bwana Rashid Madaraka amelishukuru Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kwa namna wanavyoshirikiana nao kama wafanyabiashara kwa kutoa elimu mara kwa mara kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo kutunza amani na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.

Mkaguzi Hokororo aliambatana na Mkuu wa Polisi Jamii Wilaya ya Kibaha, Wakaguzi wa kata za Maili moja, Tangini, Kongowe, Tumbi na Boko Mnemela ili kuyafikia makundi mbalimbali ya jamii ikiwemo maafisa usafirishaji na wafanyabiashara na kuwaelimisha umuhimu wa amani kwa maendeleo ya jamii.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI