Header Ads Widget

MWANAJESHI WA MAREKANI KUTOKA KENYA ASHIKILIWA KWA KUINGIA NA MABOMU NCHINI

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Tarime Rorya Novemba 16, 2025 majira ya saa sita mchana  katika eneo la Mpaka wa Tanzania na Kenya- Sirari, limethibitisha kumkamata Bw. Charles Onkuri Ongeta (30) Mwenye Uraia Pacha wa Kenya na Marekani akiwa na mabomu manne ya kurushwa kwa mkono aina ya CS- M68 akitokea Kenya kuingia Tanzania.


Kulingana na Taarifa ya Polisi kwa Vyombo vya habari iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP ) Mark Njera, Ongeta ni Mwanajeshi wa Jeshi la Marekani mwenye cheo cha  Sajenti na alikuwa akiingia nchini kwa kutumia gari yenye usajili wa KDP 502 Y, aina ya Toyota Landcruiser.

Polisi imesema mabomu hayo kulingana na sheria za nchi za umiliki wa silaha ni marufuku kuingia nchini hata kama angekuwa na kibali ambapo ushahidi unaendelea kukusanywa sambamba na kuhojiwa kwa tuhuma hizo ili hatua stahiki kwa mujibu wa sheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya mtuhumiwa huyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI