Header Ads Widget

BABA ASKOFU MPEMBWA AWAOMBA WATANZANIA KURIDHIA MARIDHIANO YA PAMOJA


  Asifu moyo na Upendo wa Rais Samia wa kuiunganisha jamii 

Baba Askofu Bethania Simon Mpembwa, Kiongozi wa Kanisa la Neema ya Kitume, Mbezi Luis Mkoani Dar Es Salaam amesema ni faraja kuona dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuendelea kulileta taifa pamoja na kutafuta maridhiano ya Taifa, akitoa wito wa kila mmoja kuitika na kushiriki katika mchakato huo wa maridhiano.

Askofu Mpembwa amebainisha hayo siku chache mara baada ya hotuba ya Rais Samia Bungeni Mjini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Bunge la 13, Novemba 14, 2025 Ijumaa ya Wiki iliyopita, akiyataka makundi mbalimbali ya kijamii kuridhia fursa hiyo ya Rais Samia ili kuweza kutoka kwenye mkwamo na changamoto iliyojitokeza.

"Tutumie dhamira yake ya 4R vyema na kila mmoja awe na moyo wa kizalendo sio moyo wa kutweza mwingine ama kushindana, kudhalilisha au kuumiza mwingine." Amesisitiza Baba Askofu.

Aidha Kiongozi huyo wa dini amerejea pia maandiko matakatifu kutoka kwenye Kitabu cha Biblia kisemacho kheri wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu, akisema kinyume chake Mungu hapendi wachonganishi bali hupenda watu wanaokaa pamoja kwa Upendo katika jamii.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI