Tim Davie amejiuzulu kama Mkurugenzi Mkuu wa BBC pamoja na afisa Mtendaji Mkuu wa BBC News, Deborah Turness, pia amejiuzulu.
Hatua hii inakuja huku Shirika hilo kubwa la habari likitarajiwa kuomba radhi kesho kufuatia wasiwasi kuhusu upendeleo wa kisiasa, ikiwemo jinsi hotuba ya Rais wa Marekani Donald Trump ilivyohaririwa katika kipindi cha Panorama.
Wasiwasi huo unahusu vipande vya video vilivyokatwa na kuunganishwa kutoka sehemu mbalimbali za hotuba ya Rais huyo wa Marekani ya tarehe 6 Januari 2021, ili kuonekana kana kwamba aliwaambia wafuasi wake angekwenda nao hadi Jengo la Bunge la Marekani (US Capitol) "kupigana kwa nguvu zote," katika makala ya Trump: A Second Chance?, iliyotangazwa na BBC wiki moja kabla ya uchaguzi wa Marekani mwaka jana.
Bwana Davie ametuma ujumbe kwa wafanyakazi jioni ya leo, akisema kwamba ilikuwa ni uamuzi wake binafsi kujiuzulu.






0 Comments