Header Ads Widget

DENI LA TAIFA LA MAREKANI LIMEPANDA HADI TRILIONI 38

 


Deni la Taifa la Marekani limepanda na kufikia Dola Trilioni 38, likiwa ndilo deni kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa katika historia ya taifa hilo, kwa mujibu wa Jarida Kuu la Uchumi Duniani.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa ongezeko hilo limechangiwa na matumizi makubwa ya kiserikali katika sekta muhimu kama ulinzi, afya, na miradi ya kijamii, huku wachambuzi wakionya juu ya athari za muda mrefu katika uthabiti wa uchumi wa taifa hilo.

Kwa mujibu wa takwimu za Hazina ya Marekani (US Treasury), mwaka 2000 deni la taifa lilikuwa takriban Dola Trilioni 5.6, lakini tangu mwaka 2019 limepanda kwa zaidi ya Dola Trilioni 15.

Wataalamu wa uchumi wanasema kasi hii ya ukuaji wa deni imetokana na sera za matumizi makubwa ya bajeti na miradi mikubwa isiyo na tija, hasa katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni.

Kwa mujibu wa viwango vya sasa vya ubadilishaji wa fedha, Dola Trilioni 38 ni sawa na takriban Shilingi Trilioni 102,600 za Kitanzania (TZS 102.6 Quadrillion) - kiwango kinachoonyesha ukubwa wa mzigo wa kifedha unaolikabili taifa hilo.

Chanzo: Jarida la Uchumi Duniani @wealth less

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI