Header Ads Widget

MBEYA NA GEITA ZILIVYOHARIBIWA KWENYE VURUGU ZA OKTOBA 29, 2025

 


NA MATUKIO DAIMA MEDIA.

Mikoa ya Mbeya na Geita ni Miongoni mwa Mikoa iliyoathirika pakubwa na ghasia na Vurugu za Jumatano Oktoba 29, 2025, leo hii Mamia ya wananchi wakiachwa na maumivu makali ya kutokana na kuteketezwa kwa rasilimali zao mbalimbali Ikiwemo magari, Vibanda vya biashara pamoja na Miundombimu mingine iliyokuwa ikituma kutoa huduma kwa wananchi.

Kulingana na mashuhuda na waathirika   wa madhila hayo, Wengi wa walioharibikiwa, kuibiwa na kuchomwa moto kwa mali zao ni pamoja na wamiliki wa magari waliokuwa wamepaki magari na wale waliokuwa wamefuata huduma ya mafuta kwenye Vituo mbalimbali vya mafuta wakati ghasia hizo zilipoibuka katika maeneo yao.


Kwa Mkoa wa Mbeya, eneo la Uyole mbali ya kuchomwa kwa mali binafsi za wananchi, miundombinu mbalimbali iliharibiwa ikiwa ni pamoja na barabara na Vibanda vya pembezoni mwa barabara, vibanda ambavyo vilikuwa vikituma kwaajili ya biashara za akinamama wajasiriamali waliokuwa wakiuza bidhaa za vyakula, mbogamboga na matunda.

Kwa Mkoa wa Geita, miongoni mwa vituo vya mafuta vilivyoathirika kwa uporaji na uchomaji wa moto ni pamoja na Vituo vya Lake energies Katoro na kile cha Nyankumbu, sambamba na nyumba za askari Polisi na Kituo cha Polisi cha Nyankumbu, ambavyo vyote viliteketea pamoja na mali zilizokuwepo ndani na nje ya majengo na Vituo hivyo.

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI