Header Ads Widget

LAKE OIL GROUP WAONGEA KWA UCHUNGU, VITUO 38 VYACHOMWA MOTO, 300 HAWANA KAZI


Jumatano ya Oktoba 29, 2025, inabaki kuwa siku yenye kumbukumbu miongoni mwa Watanzania, kwani pamoja na kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, lakini wapo wananchi waliopata madhila mbalimbali ikiwamo kujeruhiwa na kupotea huku wengine wakiharibiwa mali zao katika Majiji ya Dar es salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya, pia katika Mikoa ya Shinyanga, Geita, Songwe, Ruvuma, Mara, Dodoma, Kilimanjaro na Iringa kwa mjibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi nchini.

Kampuni ya Lake Oil Group ni miongoni mwa kampuni inayomilikiwa na Mtazania mzawa ilikumbwa na athari hasi kwani vurugu hizo zilisababisha kuharibiwa na hata kuchomwa moto kwa baadhi ya rasilimali zake.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Lake Oil Group, Stephen Mtemi ameelezea namna walivyoathirika na vurugu hizo huku akitoa pole kwa wananchi walioathirika kwa namna moja au nyingine.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI