Header Ads Widget

HUDUMA ZA KIJAMII ZATATIZIKA TUNDUMA,MAJENGO NA SAMANI ZA SERIKALI ZIKICHOMWA MOTO

 

Wananchi wa Halmashauri ya Mji wa Tunduma Mkoani Songwe ni miongoni mwa wananchi ambao hawatosahau madhila makubwa yaliyosababishwa na ghasia ma vurugu za Jumatano ya Oktoba 29, 2025 pale ambapo Magenge ya waharibifu na wezi walipovamia na kuteketeza mali na miundombinu mbalimbali ya serikali, iliyokuwa ikitumika katika utoaji wa huduma muhimu za kila siku kwa wananchi wa Eneo hilo na Mkoa mzima wa Songwe.


Katika Video na picha kadhaa, kumeonekana waandamanaji wakichoma magari ya serikali waliyoyakuta katika maeneo mbalimbali, magari zaidi ya matano yaliyokuwa Mizani ya Mpemba Tunduma, kuteketeza kwa moto jengo lililokuwa likitumika na Maafisa wanaosimamia Mizani hiyo, sambamba na kuiba na baadae kuteketeza kwa moto magari yote yaliyokuwa yamepanga foleni katika mizani hiyo kusubiria kupimwa.



Aidha waharibifu hao pia waliiba na kuchoma moto majengo na samani za Mahakama ya Mwanzo Tunduma pamoja na kuchoma vituo vya Polisi katika Mji humo muhimu kwa biashara na shughuli za Kijamii Mkoani Songwe.


Kwasasa wananchi hao wameendelea kutaabika na kukosekana huduma muhimu za kijamii katika eneo hilo licha ya serikali kuwa tayari imerejesha amani na utulivu katika eneo hilo, wakisubiri ujenzi na ukarabati wake ili huduma za utoaji haki na usimamizi wa sheria na taratibu za barabara kuweza kuendelea kama ilivyokuwa awali kabla ya ghasia na vurugu za Jumatano ya Oktoba 29, 2025.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI