na Hamida Ramadhani.
Bi. Christina Kazimoto, Mama na Mjasiriamali anayefanya shughuli zake za kiuchumi Jijini Dar Es Salaam, ametoa wito kwa wazazi na walezi kuketi pamoja na Vijana na watoto wao na kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa amani na wajibu wa kila mmoja katika kuilinda na kuienzi amani kama msingi muhimu wa ustawi na maendeleo yao.
Bi. Kazimoto ameyaeleza hayo kufuatia taarifa mbalimbali na hamasa za uvunjifu wa amani, vurugu na ghasia zinazoendelea kwenye Mitandao ya kijamii nchini, akiwataka Vijana kutoshawishika na yale yanayoendelea katika Mataifa mengine duniani, akisema si wote wanaofurahia amani, upendo na mshikamano wa Watanzania yaliyopo sasa.
Amealaani pia kilichotokea Oktoba 29, 2025 siku ya uchaguzi Mkuu na baada ya uchaguzi Mkuu, akisena Watanzania walizoea amani na tukio lile ni jambo asilotamani liweze kujirudia tena nchini.
"Ilifika mahali hakuna usafiri, huduma za chakula zilikuwa shida, maduka mengi yalifungwa wakihofia uvunjifu wa amani, mchele tuliokuwa tunanunua 2,000 tulinunua 5,000 na hata bodaboda pale tulipokuwa tunaenda kwa 1, 000 tulienda kwa 5, 000. Tumejifunza umuhimu wa amani na niombe Vijana wasishawishike tena kuhusu kuhatarisha amani."Amesema Bi. Kazimoto.
Aidha Mwananchi huyo pia amehimiza matumizi ya njia sahihi katika utafuta wa haki ikiwemo mazungumzo kati ya wanaosumbuka na kero mbalimbali pamoja na Viongozi wao, akisema hakuna jambo lisiloweza kupatiwa ufumbuzi wake kwa njia ya amani na ya mazungumzo.






0 Comments