Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Mhe. Johnston Mutasingwa, ametoa wito kwa Wananchi wa Bukoba na Watanzania kwa ujumla kuendelea kuilinda amani ambayo taifa limeidumisha kwa muda mrefu.
Mhe. Mutasingwa ametoa wito huo leo, tarehe 28 Desemba 2025, wakati wa kikao cha Baraza la Biashara la Wilaya kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba ikiwa ndio kikao chake cha kwanza tangu ameapishwa kuwa mbunge wa jimbo hilo
Akizungumza katika kikao hicho, alisema, suala la amani ni suala ambalo kila mmoja anatakiwa kuhusika nalo kwa sababu bila amani hatuwezi kuyafanya haya yote tunayoyafanya.
“Sisi leo tumekaa kujadili mambo mbalimbali na fursa za kibiashara zinazopatikana katika wilaya yetu niseme tu ukweli bila amani tusingeweza kukaa hivi pamoja na pia tusingeweza kufanya biashara,” alisema Mhe. Mutasingwa.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Mhe. Erasto Sima, amesisitiza umuhimu wa kudumisha amani, akibainisha kwamba machafuko hayajawahi kuleta matokeo chanya katika jamii. “Tuilinde amani ya nchi yetu kwa sababu ndiyo nguzo ya maendeleo ya taifa,” alisema Erasto





0 Comments