NA MATUKIO DAIMA MEDIA,DODOMA
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kuwasisitiza Watanzania kuliombea Taifa ili amani, upendo, ustahimilivu na mshikamano viendelee kudumu.
Waziri Dkt Nchemba amesema hayo leo, Jumapili Novemba 16, 2025, alipowasilisha salamu za Mheshimiwa Rais kwa waumini na viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kisasa, mkoani Dodoma.
"Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anawasalimu sana. Yuko pamoja nanyi, na rai yake kwa Watanzania ni kuendelea kufanya maombi kwa ajili ya Taifa letu ili liendelee kuwa tulivu," amesema.
Aidha, Waziri Mkuu amesema ni wajibu wa kila Mtanzania kulinda na kuenzi amani, kwani bila amani taifa haliwezi kutekeleza majukumu yake, ikiwemo kuabudu na kuendesha shughuli mbalimbali za kijamii.
"Pasipo amani hatuwezi kutekeleza majukumu yeyote. Pasipo amani hatuwezi kuendesha ibada. Kwa hiyo ni wajibu wa kila Mtanzania kuiombea nchi yetu. Pakiwa na amani tunaweza kutekeleza matarajio yetu, na hata kutatua yale tunayoyaona kuwa magumu,” amesisitiza








0 Comments