Header Ads Widget

BUNGE LA ULAYA LAPITISHA AZIMIO HILI KWA TANZANIA

 

Bunge la Ulaya limepitisha azimio la kuitaka Kamisheni ya Umoja wa Ulaya (EU) kusitisha mpango wa ufadhili kwa Tanzania baada ya ghasia za uchaguzi kusababisha mauaji ya raia na uharibifu wa mali katika miji mbalimbali nchini humo.

Bunge hilo pia limepitisha azimio lenye vipengele tisa ikiwemo kukemea mauaji baada ya uchaguzi na hali ya haki za binadamu nchini Tanzania, pamoja kesi ya kiongozi wa upinzani, Tundu Lissu.

Hata hivyo maamuzi na jukumu kuu la kusitisha ama kuendelea kuifadhili Tanzania lipo mikononi mwa Kamisheni hiyo ya EU, Bunge katika vikao vya leo Alhamisi liliazimia kwamba mpango wa kila mwaka wa AAP wa kufadhili Tanzania mwaka wa 2025 haupaswi kukubaliwa kuendelea.

Awali Ubalozi wa Tanzania huko Brussels, Ubelgiji lilipo Bunge la Ulaya ulieleza wasiwasi wake kuhusu uamuzi wa Bunge hilo kuandaa mjadala huu bila kushirikisha upande wa pili yaani Serikali ya Tanzania.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI