Na Lilian Kasenene MorogoroMatukio DaimaApp
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umeanza utekelezaji wa mpango wa kuimarisha mifumo ya kidigitali nchini, ukiwalenga watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara, kwa lengo la kuongeza ufanisi wa utoaji huduma, kulinda haki za wamiliki wa biashara, na kuchochea ukuaji wa uchumi wa viwanda.
Akizungumza mjini Morogoro katika kikao kazi Cha Viongozi, Watumishi na menejimenti ya Wizara ya Viwanda na Biashara Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk Hashil Abdallah, aliwataka kuhakikisha wanatafsili kwa vitendo maelekezo ya Serikali ya awamu ya sita uboreshaji wa Mazingira ya ufanyaji wa biashara.
Mafunzo hayo ya utekelezaji wa mifumo ya kidigitali unalenga kuwajengea uwezo watumishi wa umma na sekta binafsi kutumia teknolojia kwa ufanisi zaidi, ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za usajili wa kampuni, alama za biashara na leseni.
Katibu mkuu huyo alisema jukumu la Brela ni kutekeleza sera ambazo zinasimamiwa na Wizara hivyo uelewa wa pamoja ndani ya kikao kazi hicho itajenga msingi imara ya uwajibikaji na usimamizi katika kutekeleza sera ya Taifa ya biashara na sera ya Maendeleo endelevu.
"Nataka mjadili kwa kina utoaji wa leseni za biashara na leseni za viwanda zenye mawanda, changamoto kama zipo na mifumo iliyopo ndani ya Wizara,"alisema Dk Abdallah.
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Godfrey Nyaisa, alisema taasisi hiyo inaendelea kuimarisha mifumo ya kidigitali ili kupunguza urasimu, kulinda haki za wamiliki wa biashara, na kuhakikisha wananchi wanasajili biashara zao kwa usalama kupitia mtandao.
"Hii ni sehemu ya muelekeo wa serikali katika kujenga uchumi wa kidigitali na kuimarisha mazingira rafiki ya uwekezaji nchini,"alisema Nyaisa.
Alisema mafunzo kwa viongozi hao yameandaliwa kwa lengo la kutoa Elimu ya kina na kuhakikisha Watumishi hao wanafahamu kwa undani majukumu ya Brela l, taratibu za usajili na utoaji wa leseni pamoja na mafunzo ya mifumo ya kidigitali ili wawe mabalozi Waziri kwa kutoa ushauri wa kibiashara.
"Brela ni taasisi muhimu katika ico system ya biashara nchini ikisimamia utekelezaji wa Sheria kuu sita,"alisema.
Mwenyekiti wa Bodi BRELA Prof. Neema Mori alisema kama Bodi wanatambua umuhimu wa uwepo wa mafunzo na kwamba wataendelea kusimamia Brela na kuhakikisha inatimiza malengo ambayo wamejiwekea ili kuwa na ufanisi wa kuboresha biashara na kuwa wabunifu.







0 Comments