Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania IGP Camillus Wambura amesema miongoni mwa changamoto watakazokutana nazo wahitimu wapya wa mafunzo ya awali ya Polisi ni pamoja na matishio ya ugaidi wa dunia, uwepo wa dawa za kulevya, usafirishaji haramu wa binadamu na uhamiaji haramu.
IGP Wambura amebainisha hayo Moshi Mkoani Kilimanjaro alipokuwa akifunga mafunzo ya awali ya Polisi kwa Kozi namba moja ya mwaka 2024/25, akisema kazi za Polisi zinahitaji ushirikiano wa dhati na wa karibu ili kuweza kuzuia na kupambana na changamoto hizo.
IGP Wambura pia akisisitiza kuhusu umuhimu wa usalama kama nyenzo ya maendeleo na ustawi wa Binadamu, ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuweza kudhibiti uhalifu na wahalifu kote nchini Tanzania.
" Tusikubali pia kugawanyika kutokana na sababu yeyote ile iwe ya kisiasa, kidini au rasilimali. Tuendelee kutunza tunu yetu ya usalama na amani ya nchi yetu iliyodumu takribani kwa miongo mingi sasa. Tushirikiane popote kuhakikisha tunakuwa salama." Amesisitiza IGP Wambura.
Awali wakati wa maelezo yake, Mkuu wa Chuo hicho Ramadhan Mungi amesema askari wapya 4, 826 wakiwemo wanaume 3, 436 na wanawake 1, 390 wamehitimu mafunzo hayo, huku wanafunzi 217 wakiondolewa chuoni hapo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa nidhamu na uwezo mdogo katika kujifunza.





.jpg)





0 Comments