Header Ads Widget

WAKAZI WA GAZA BADO WAKO KATIKA "HALI MBAYA" – SHIRIKA LA MSF

 

Mratibu wa huduma za dharura huko Gaza wa shirika la Médecins Sans Frontières (MSF), amesema  kwamba watu katika Jiji la Gaza wanaishi katika "hali mbaya" huku kukiwa na upungufu wa chakula, maji na huduma za afya.

MSF imelazimika kusitisha "shughuli muhimu za matibabu" katika jiji la Gaza mwishoni mwa Septemba, ambayo Granger anasema ilitokana na kuzorota kwa hali ya usalama na kuongezeka kwa mashambulizi ya anga.

Mfanyikazi wa MSF Omar Hayek aliuawa huko Gaza siku ya Alhamisi, mwanachama wa 14 wa MSF kuuawa huko Gaza tangu 7 Oktoba 2023.

"Hili ni jukumu kutoka kwa mamlaka ya Israeli, unapaswa kulinda misheni ya kibinadamu," Granger anasema, akielezea "siku ngumu" kufuatia kifo cha mwenzake.

"Wahudumu wa misaada ya kibinadamu hawajalindwa, fikiria hali ikoje kwa raia wengine wote."

Na wenyeji wanatamani sana kujua ikiwa hatua za hivi punde za kisiasa zinamaanisha mwisho wa vita

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI