Header Ads Widget

WAANDISHI WA HABARI WAASWA KUIMARISHA UADILIFU WAKATI WA UCHAGUZI MKUU.

 

Na Shemsa Mussa -Matukio Daima 

Kagera.

 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kagera,   imewataka waandishi wa habari kuhakikisha wanatumia vyema kalamu zao kuwaelimisha wananchi kuhusu madhara ya rushwa, hususan katika kipindi cha uchaguzi mkuu. 

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa ofisi za TAKUKURU mkoani humo leo, Bw Vangsada Mkalimoto,Amesema waandishi wa HABARI, wana nafasi kubwa katika kuelimisha jamii hivo ni vema kuwaelimisha Wananchi madhara yatokananyo na rushwa.

inatambua thamani ya kura na wajibu wa kuwapata viongozi waadilifu. Mkalimoto Amesema waandishi wana nafasi kubwa katika kuhakikisha jamii inatambua thamani ya kura na wajibu wa kuwapata viongozi waadilifu.

Aidha, aliwasisitiza waandishi wa habari kutumia taaluma yao kuhamasisha uwajibikaji wa viongozi na uwazi katika mchakato wa uchaguzi, badala ya kuwa sehemu ya mifumo ya upotoshaji au upendeleo. 

“Kupambana na rushwa si jukumu la TAKUKURU pekee, bali ni jukumu la kila mwananchi, hususan wanahabari ambao sauti zao zinasikika zaidi katika jamii,”Kila mwandishi wa habari anatakiwa kuwa na elimu, maarifa na uelewa mpana wa masuala mbalimbali kila siku, ili kurahisisha kazi yake ya kuelimisha jamii kwa ufanisi,” amesema Mkalimoto.

Ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kuelewa kuwa kupokea au kutoa rushwa wakati wa uchaguzi ni kuharibu haki yao ya msingi ya kuchagua kiongozi bor huku akisema moja ya changamoto kubwa inayowakabili ni uelewa mdogo wa wananchi kuhusu rushwa na athari zake katika maendeleo ya taifa Alibainisha kuwa elimu endelevu kwa umma kupitia vyombo vya habari ni silaha muhimu ya kuzuia vitendo vya rushwa kabla havijajitokeza.

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria semina hiyo, akiwemo Sylivia Amandius na Annod Kailembo, walisema mafunzo hayo yamekuwa chachu ya kuwakumbusha wajibu wao katika kipindi muhimu cha uchaguzi. Walisema watatumia majukwaa yao kufikisha elimu sahihi kwa wananchi kuhusu athari za rushwa na umuhimu wa kushiriki uchaguzi kwa uwazi.

Semina hiyo iliandaliwa na TAKUKURU kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi hiyo na vyombo vya habari, sambamba na kuongeza uelewa wa wanahabari kuhusu mbinu za kuzuia na kuripoti vitendo vya rushwa vinavyoweza kujitokeza katika kipindi cha uchaguzi mkuu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI