Header Ads Widget

VIJANA LINDI WAHIMIZWA KUJIUNGA NA NSSF KUNUFAIKA NA MAFAO YA HIFADHI YA JAMII


VIJANA Mkoani Lindi wametakiwa kuacha dhana potofu ya kuwa wanaostahili kunufaika na mifuko ya hifadhi ya jamii ni wazee wastaafu pekee badala yake wamehimizwa kujiunga na mifuko hiyo kupitia hifadhi ya skimu kutoka mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF ili kunufaika na mafao mbalimbali 

Akizungumza kwa niaba ya wanachama wengine wasio na ajira rasmi na wachangiaji wa hifadhi ya skimu kutoka NSSF Mkoani humo wakati wa kuhitimisha Wiki ya huduma kwa wateja 2025 Bonifasi Chogo amesema upo Umuhimu kwa vijana kujiunga na mfuko huo kwani faida nyingi wanazoweza kuzipata sawa na wale waliojiunga kwa mujibu wa Sheria

Amesema kwa vijana na Watu wasio na ajira rasmi wanaweza kunufaika na mafao mbalimbali kama vile, fao la pesheni ya uzeeni, uzazi, huduma za Afya, na gharama za mazishi

Kaimu Meneja wa mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF Mkoa wa Lindi Saad Haji Amesema kupitia wiki hiyo ya huduma kwa wateja  umefanikiwa kuwafikia wanachama katika halmashauri zote za mkoa huo na kuwapatia elimu ya huduma za kidijitali.

Kaimu Meneja wa NSSF Lindi, amesema kuwa kwa sasa wanachama na waajiri wanaweza kupata huduma mbalimbali kwa njia ya mtandao bila kulazimika kufika ofisini.

Kauli mbiu ya wiki ya huduma kwa wateja kimataifa ni Mpango umewezekana huku mfuko wa hifadhi ya jamii ikibeba kaulimbiu isemayo kidigital tumeweza ikijivunia hatua kubwa iliyopigwa Katika utoaji wa huduma kwa mfumo wa Tehama 



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI