Header Ads Widget

SONGWE KUFANYA UCHAGUZI WA MFANO– RC MAKAME.

 

Na Moses Ng’wat, Tunduma.  

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Jabiri Omary Makame, amewahakikishia wananchi wa mkoa huo kwamba, amani na utulivu vitadumishwa wakati wote wa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025, huku akiwataka wajitokeze kwa wingi kutumia haki yao ya kikatiba kupiga kura na kuwachagua viongozi wanaowataka.  

madereva wa bajaji, bodaboda pamoja na wananchi wa Mkoa wa Songwe kupitia vyombo vya habari vilivyokuwa vikirusha moja kwa moja mkutano wake uliofanyika katika eneo la Kisimani ambalo ni kitovu cha biashara cha Mji wa Tunduma, wilayani Momba.  

Amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vimejipanga kuhakikisha hali ya amani inatawala wakati wa uchaguzi na hata baada ya kumalizika kwa zoezi hilo.  

"Wananchi wenzangu hakuna haja ya kuwa na hofu, tujitokeze kwa wingi kupiga kura kwa amani na kutumia haki yetu ya msingi kuchagua viongozi wanaofaa kutuongoza kwa miaka mitano ijayo,” amesema Makame.  

Aidha, amewaonya watu wachache wanaopanga au kushawishi vurugu wakati wa uchaguzi, akisisitiza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vipo macho na vitachukua hatua kali kwa yeyote atakayevunja sheria.  

Mkuu huyo wa mkoa amebainisha kuwa, maendeleo ya Mkoa wa Songwe yanategemea uongozi bora, hasa katika sekta za kilimo, biashara ndogondogo na huduma za kijamii, huku akisisitiza kuwa hata makundi kama machinga na waendesha bodaboda ustawi wa kazi zao hutarajia uamuzi wa viongozi wanaochaguliwa katika ngazi mbalimbali za utawala.  

" Vijana wenzangu na wananchi kwa ujumla, tuilinde amani yetu, jukumu la kulinda amani si la vyombo vya dola pekee, bali ni letu sote.... tukiona dalili za uvunjifu wa amani, tuchukue hatua kwa kutoa taarifa mapema,” amehimiza Makame.

Akizungumzia maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2025, Makame amesema Mkoa wa Songwe umeendelea kushiriki kikamilifu katika hatua zote zinazosimamiwa na Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania (INEC), huku wananchi wakiendelea kuonyesha mwamko na ushirikiano mkubwa katika maandalizi hayo — jambo linaloashiria uchaguzi wa amani na utulivu.  

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva Bodaboda wa Mji wa Tunduma, Paulo Mjwang maarufu kwa jina la Magufuli, amewataka vijana wenzake kuepuka kurubuniwa na watu wanaotaka kuvuruga uchaguzi, badala yake washiriki ipasavyo katika kupiga kura kwa amani na utulivu.  

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI