Mgombea Ubunge wa Jimbo la Isimani kupitia CCM,William Vangimembe Lukuvi ameendelea na kampeni zake leo kwa kutembelea vijiji vinne vijiji vitatu kutoka Kata ya Mboloboli na kijiji kimoja cha Mapera Mengi kutoka Kata ya Migori.
Katika mikutano hiyo, Lukuvi amesisitiza umuhimu wa wananchi kujitokeza kwa wingi tarehe 29 Oktoba 2025 kupiga kura kwa Rais, Mbunge na Diwani wa CCM ili kuendeleza kasi ya maendeleo chini ya uongozi wa *Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa Vijijini Constantine Kihwele ameshiriki mikutano hiyo, akiungana na Lukuvi kunadi Ilani ya CCM na wagombea wa ngazi zote.
Huku akisisitiza kuwa CCM inaendelea kujipambanua kwa maendeleo ya vitendo na ndiyo njia sahihi ya kulinda na kusukuma mbele mafanikio yaliyopatikana.
0 Comments