NA Hadija Omary.
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Lindi, wametoa msaada wa vyakula na mahitaji mbalimbali kwa watoto wenye mahitaji maalumu wa shule ya msingi Nyangao halmashauri ya Mtama kama sehemu ya kuadhimisha siku ya huduma kwa wateja
Tukio hilo limefanyika Jana huko Katika viwanja vya shule ya msingi Nyangao ambapo miongoni mwa vitu vilibyokabidhiwa ni pamoja na Unga, mchele, sukari, mafuta na sabuni
Akizungumza Mara baada ya kufanya makabishiano hayo Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja kutoka Tanesco Mkoa wa Lindi, Robert Fredy, Amesema imekuwa NI desturi kwa Shirika hilo kitoa msaada kwa Makundi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kurejesha kwa jamii.
Aidha Amesema katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, shirika limeona ni vyema kurejesha kwa jamii sehemu ya kile kidogo walichokipata kutokana na huduma wanazotoa kwa wateja wake.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyangao, Richard Mponda, ameishukuru TANESCO kwa msaada huo, huku Akieleza kuwa msaada huo utaenda kuongeza Hali ya kujifunza kwa wanafunzi
Hata hivyo mwalimu mponda ametoa wito kwa Taasisi zingine za ndani na Nje ya Mkoa kujitokeza na kulisaidia kundi hilo ambalo bado lina mahitaji ya msingi kama chakula na vifaa vya kitaaluma
baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wameeleza kufurahishwa na msaada huo, ambapo wameeleza kuwa utawasaidia kuendelea na masomo yao kwa Hari
Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja hufanyika kila mwaka yakiwa na lengo la kuimarisha uhusiano kati ya taasisi na wananchi wanaonufaika na huduma hizo ambapo kwa mwaka huu imebeba ujumbe wa "Mpango umewezekana"
0 Comments