Na Mariam Kaagenda _Kagera
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ngara Dotto Jasson Bahemu amewataka Wananchi wa Jimbo hilo wenye sifa za kupiga kura kujitokeze kwa wingi tarehe 29 Oktoba, 2025 kumchagua Rais, Mbunge na Madiwani .
Akizungumza na Wananchi katika mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Kata ya Bukiriro, mgombea huyo wa Ubunge ameomba kura za Mgombea Udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi Bwana Erick Emily Nkilamachumu, kura za Mbunge Dotto Jasson Bahemu na Kura za mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Bahemu amesema kuwa zoezi la upigaji wa kura ni haki kwa kila Mtanzania mwenye sifa za kupiga kura hivyo wananchi wa Jimbo la Ngara wanatakiwa kujitokeza kwa wingi katika vituo vya kupigia kura walivyojiandikishia ili kutimiza haki yao
Akiomba kura za Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bahemu amesema katika kipindi cha Miaka 4 Rais Samia amefanya mambo mengi ya maendeleo kupitia miradi iliyogharimu takribani kiasi cha shilingi bilioni 81.
Aidha, amewataka Wananchi wote kuhakikisha wanapiga kura za ndiyo kwa wagombea wote wa Chama Cha Mapinduzi ili waweze kuharakisha maendeleo ya Jimbo hilo
0 Comments