Header Ads Widget

SIRRO ATAKA WANANCHI KUTOA USHAHIDI KESI ZA UKATILI

 

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MKUU wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro amewataka wananchi wa mkoa Kigoma kujitokeza kutoa ushahidi wa kesi za matukio ya ukatili ili mahakama ziweze kutoa hukumu ya haki kwa watu wanaokutwa na hatia ya vitendo hivyo kwani kwa sasa watuhumiwa wengi wanaachiwa kwa mahakama kukosa ushahidi dhidi yao.


Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro (kulia aliyesimama) akizungumza na wananchi waliofika dawati la jinsia la polisi wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma

Balozi Sirro ametoa kauli hiyo wilayani Kasulu mkoani Kigoma aalipotembel;ea na kuzungumza na watendaji wa dawati la jinsia la jeshi la polisi wilayani Kasulu na kubainisha kuwa kuendelea kuwepo kwa vitendo vya ukatili katika jamii kunachangiwa kwa kiasi kikubwa jamii yenyewe kushindwa kutosha ushahidi unaotosheleza kuwatia hatiani watuhumiwa.

Akiwa katika ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa chini ya Program ya Pamoja ya Kigoma (KJP) inayotekelezwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Balozi Sirro alisema kuwa athari ya jamii kutokuwa tayari kutoa ushahidi wa kesi za ukatili na badaala yake mambo hayo kumalizwa kijamii kumesababisha matukio ya ukatili kuendelea mkoani humo.

Mkuu wa Dawati la jinsia la jeshi la polisi wilayani Kasulu,Sperius Rweyemamu (kushoto) akitoa taarifa ya utendaji wa dawati kwa mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro (aliyekaa kulia)

 Pamoja na changamoto hiyoMkuu huyo wa mkoa Kigoma ameitaka jamii  kudumisha malezi bora na yenye maadili  kwa watoto hali itakayopunguza matukio ya ukatili Sambamba na kutoa wito kwa watendaji wa dawati la jinsia la jeshi la polisi kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia utu na misingi ya sheria ili kulifanya dawati hilo kuwa kimbilio kwa wananchi wenye changamoto za vitendo vya ukatili. 

Awali Mkuu wa Dawati la jinsia la jeshi la polisi wilayani Kasulu,Sperius Rweyemamu,alisema kuwa dawati hilo limesaidia kukabiliana na vitendo vya ukatili na unyanyasaji kijinsia wilayani humo ikiwemo vipigo, ubakaji na mulawiti ambavyo kipindi cha nyuma jamii ilikuwa inaaona kama jambo la kawaida.


Baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali, polisi na  Umoja wa Mataifa walioongozana na Mkuu wa mkoa Kigoma kwenye ziara hiyo

Mratibu huyo wa dawati alitaja sababu zinazochangia kukwama kwa kesi za matukio ya ukatili wilayani humo kuwa ni pamoja na matukio kuamuliwa kwa ngazi ya jamii, uchelewaji wa kutoa taarifa Zaidi ya masaa 72 ya kisheria, wananchi kushindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi kwa kisingizio cha kukosa nauli na wakati mwingine ndugu wa waathirika kudai fedha kutoka kwa watuhumiwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI