Mgombea ubunge jimbo la. Kigoma Mjini kwa Cjama Cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Mwanga Community Centre Mjini Kigoma
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma Zitto Kabwe amesema kuwa miaka 15 ambayo amekuwa mbunge katika majimbo mawili ya mkoa Kigoma amejenga heshima kwa wananchi wa mkoa huo ambapo sasa wanatembea na kuona ufahari kutangaza wanatoka Kigoma.
Zitto amesema hayo akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika viwanja vya Mwanga Community Centre Mjini Kigoma na kusema kuwa amejenga heshima na utu kwa watu wa mkoa Kigoma na kujiona kuwa sasa siyo raia daraja la pili.
Mgombea Ubunge jimbo la Kigoma Mjini ACT Wazalendo Zitto Kabwe (katikati mwenye kofia) na viongozi wa chama hicho wakitembea kwa miguu kuelekea viwanja vya Mwanga Community Centre ambapo Mgombea ubunge huyo alihutubia wananchi
Mgombea huyo akisema juwa pamoja na kujenga kujiamini na kuwafanya kuwa watu wanaojenga hoja pia kwa maisha yake ya siasa amepigania changamoto ya watu wa mkoa huo kuonekana siyo raia akitaka uwepo wa usawa katika jambo hilo kama inavyofanywa mikoa mingine ambayo inapakana na nchi jirani.
" Hata sasa nikifuata amrita ya Mungu (kufa) nitakwenda nikitabasamu kutokana na kazi kubwa niliyofanya kuwapigania wananchi wa mkoa Kigoma na sitaacha hadi uhai wa maisha yake, hivyo nichagueni niendelee kupigania maendeleo ya maisha yenu," Alisema Zitto Kabwe.
Akieleza miaka mitano aliyokuwa mbunge jimbo la Kigoma Mjini (2015 - 2020) alisema kuwa kwa kusaidiana na idadi kubwa ya madiwani na meya waliyokuwa nayo walifanya kazi kubwa ikiwemo kuimarisha barabara za manispaa ya Kigoma Ujiji, kuimarisha biashara kwa kujenga masoko na kuanzisha miradi ambayo imekuwa na chachu kubwa ya kujenga uchumi wa wananchi wa manispaa hiyo.
0 Comments