Mahakama Kuu nchini Uganda imetupilia mbali ombi la kutaka nchi hiyo itoe taarifa za Wakenya wawili waliopotea nchini humo baada ya mamlaka kusema kuwa haina taarifa zao.
Mahakama ilitupilia ombi la kuitaka ishurutishe serikali kutoa taarifa kuhusu Nicholas Oyoo na Bob Njagi na kutoa ushauri wa kuripoti katika polisi ya Uganda kuhusu mtu aliyepotea.
Mahakama ilifahamishwa kuwa wawili hao walikamatwa na jeshi mnamo Oktoba 1, 2025, wakiwa kwenye kampeni na mgombea urais Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine katika wilaya ya Kaliro.






0 Comments