Na Hadija Omary
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Nachingwea Mkoani Lindi kupitia chama cha mapinduzi CCM Bwana Fadhiri Liwaka Leo amefunga rasmi kampeni zake za kusaka Kura za Rais, wabunge na Madiwani huku akiahidi kushirikiana na wananchi wa Jimbo hilo Katika shughuli za kimaendeleo ikiwa pamoja na kusimamia ujenzi wa barabara ya Nachingwea Masasi kwa kiwango cha lami
Liwaka amefunga kampeni hizo Leo oktoba 27/2025 Katika viwanja vya mauridi katika Kata ya Nachingwea Wilayani humo ikiwa ni saa chache kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika hapo kesho
Liwaka alitaja vipaumbele vyake sita ambavyo ni kutatua tatizo la maji, barabara , huduma za Afya, jenzi wa madarasa ambavyo atashirikiana na wananchi wa Jimbo hilo mara baada ya kuchaguliwa kwake na kuapishwa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo
Ikumbukwe kuwa Fadhiri Liwaka nigombea pekee wa Ubunge Katika Jimbo Hilo la Nachingwea












0 Comments