Header Ads Widget

MAMLAKA ZIKAHESHIMU MAAMUZI YA WANANCHI- ASKOFU MWANKUGA

Baba Askofu wa Kanisa la Moravian Jimbo la Mashariki Askofu Lawi Mwankuga amesisitiza umuhimu wa Watanzania kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura hapo Kesho Jumatano Oktoba 29, 2025 na kutanguliza wajibu wa kulinda amani ya Tanzania, akisisitiza kuwa Uchaguzi ni tukio la wakati mmoja na maisha ni lazima yaendelee.

Baba Askofu Mwankuga ametoa wito huo leo Jumanne Oktoba 28, 2025 Jijini Dar Es Salaam punde baada ya Vyama vya siasa kuhitimisha Kampeni zao, tayari kwa uchaguzi Mkuu, akisisitiza pia wanasiasa wanaowania nafasi mbalimbali kuyaishi yale yatakayoleta maendeleo kwa Watanzania sambamba na kutanguliza mbele maslahi yao pale watakapoibuka na ushindi wa kura za wananchi katika uchaguzi huo.


Baba Askofu amesisitiza pia umuhimu wa kuchagua kiongozi mwenye dhamira ya dhati katika kuwaletea watanzania maendeleo katika nafasi ya Udiwani, Ubunge na Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kujali Chama anachotokea Mgombea wa nafasi hizo zinazowaniwa hapo kesho.


Amewashukuru pia na kuwapongeza Watanzania kwa kujitokeza kwa wingi kwenye kujiandikisha kwenye daftari la mpigakura na uhakiki wa taarifa zao, akisisitiza pia mamlaka kuheshimu maamuzi ya wapiga kura pale watakapoamua kumchagua Kiongozi fulani kuweza kuwaongoza kwa miaka mitano ijayo mpaka pale utakapofanyika uchaguzi Mwingine mwaka 2030.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI