Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma Mjini kwa Chama Cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefunga kampeni na kusema kuwa Kigoma Mjini inamuhitaji kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo na kuondoa changamoto zao.
Zitto alisema hayo akifunga Mkutano wa kampeni katika viwanja vya shule ya Msingi Ujiji manispa ya Kigoma Ujiji na kusema kuwa siku 60 za kampeni zimemfikisha karibu na wananchi wa jimbo hilo na kujua matatizo yao.
Zitto alitaja changamoto hizo ni kwa watu wengi kushindwa kumudu gharama za matibabu hasa wale wanaopatwa na ugonjwa wa kiharasi (Stroke) n magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo yanahitaji huduma za matibabu za hospitali z rufaa.
Kutokana na hilo alisema kuwa akiwa mbunge atatoa kiasi cha Bilioni moja kuanzisha huduma za bima ya matibabu kwa wananchi wa jimbo hilo ili waweze kupata huduma za matibabu zinazostahiki.
Sambamba na hilo amelishukuru jeshi la polisi kwa kuwalinda kipindi chote cha kampeni na kuwavumilia ambapo kwa muda wote hakuna changamoto yeyote iliyotokea baina yao licha ya kuzidisha muda wa kumaliza kampeni.
Pamoja na hilo Mgombea huyo ameitaka Tume huru ya Taifa ya uchaguzi kusimamia ziezi hilo kwa uhuru na haki na kumtangaza mgombea atakayeshinda kihalali na kwamba matokeo ya halali ambayo wananchi wataamua atayakubali.
Mwisho








0 Comments