Mgombea Urais wa Chama cha NRA akihitimisha kampeni zake katika uwanja wa Community Centre mjini Kigoma
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
MGOMBEA Uraisi wa Chama Cha National Reconstruction Alliance (NRA) Almas Hassan Kisabya amesema kuwa akichaguliwa kuwa Rais wa Tanzania atapunguza ukubwa wa baraza la mawaziri ili kupunguza mzigo wa matumizi kwa serikali.
Kisabya alisema hayo akihitimisha mikutano yake ya kampeni ya Uraisi alipofanya mkutano kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre mjini Kigoma na kubainisha kuwa baraza la sasa la mawaziri linaigharimu serikali kiasi kikubwa cha fedha katika uendeshaji wake.
Alisema kuwa pamoja na kuwa na baraza kubwa la mawaziri sehemu kubwa ya mawaziri waliopo wamekuwa wakifanya mambo kwa kuwaza uchaguzi ujao badala ya kutumia utaalam walionao na nafasi zao katika kuwatumikia watanzania.





0 Comments