Header Ads Widget

KILENZI AHAMASIAHA WANANCHI KUPIGA KURA NA KULINDA MIRADI YA SERIKALI.


 NA CHAUSIKU SAID 

Wananchi wamehimizwa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29, 2025, kwa kupaza sauti zao kupitia sanduku la kura badala ya kufikiria maandamano yanayoweza kusababisha madhara makubwa.


Wito huo umetolewa na Wakili Willbard Kilenzi, wakati akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake jijini Mwanza na kusisitiza kuwa kulinda usalama wa nchi sio jukumu la polisi au vyombo vya dola pekee, bali ni jukumu la kila mwananchi.


Kipenzi ameeleza kuwa Maandamano yanaweza kisababisha uharibifu wa Mali za raia miundombinu, na kusababisha vifo visivyotarajiwa, majeruhi, na watoto kubaki yatima.


Aliongeza kuwa badala ya maandamano, wananchi wapaswa kusikiliza kampeni za vyama vyote na kuchagua ilani zao kwa makini ili kupata Serikali inayowakilisha matakwa ya wananchi wengi.


Hata hivyo amefafanua kuwa katika nchi zote za kidemokrasia, matokeo ya kura ndicho kigezo cha kwanza cha chama kuunda Serikali iliyo imara katika Taifa pia aliongeza kuwa uchaguzi ni njia ya kila raia kupaza sauti yake na kuhakikisha viongozi wanaowachagua wanatimiza ahadi zao.


“Nawaomba wanaohamasisha maandamano kutumia nguvu hizo kuwashawishi wananchi kujitokeza kupiga kura badala ya maandamano. Njia hiyo ndiyo ya kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na matokeo yake yanaheshimiwa.”

Katika hatua nyingine Kilenzi aliwaonya watumishi wa umma wanaotoa nyaraka za serikali walizopewa na kuzitumia vibaya kuzihariri na kuleta taharuki kwenye jamii ikionesha kuwa wamesahau viapo vyao, maadili ya kazi jambo ambalo ni kosa kisheria.

“Watumishi wasiofuata maadili wanaharibu mali za umma na kuchochea mfarakano wa nchi. Hatua za kinidhamu na kisheria zinahitajika kwa wale wasiotekeleza majukumu yao,” alisema Kilenzi.

Alisisitiza kuwa watendaji waliopatiwa dhamana ya kusimamia miradi hiyo wanapaswa kufanya kazi kwa ufanisi, kwani Rais hawezi kufika kila sehemu kuhakikisha miradi inafanikishwa.

Kilenzi ameishauri jamii kuchukua jukumu la kulinda amani na kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi. Aidha, aliwatahadharisha watendaji wa Serikali kuhakikisha miradi ya maendeleo inafanyiwa kazi ipasavyo ili wananchi wanufaike.

“Kupiga kura si tu haki, bali ni jukumu la kila raia kuhakikisha nchi inaendelea kuwa salama na miradi inatekelezwa,” Alisema Kilenzi.


                                     

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI