Header Ads Widget

HATUTOWAACHA SALAMA WANAOPANGA KUVURUGA UCHAGUZI MKUU- RC SENDIGA

 

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbeth Sendiga ameonya Vikali wale wote ama Vikundi vinavyopanga au kuratibu kufanya vurugu na fujo wakati wa Oktoba 29, 2025, siku ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, akiwahakikishia wananchi wa Mkoa huo usalama na mazingira tulivu kuanzia sasa, siku ya upigaji kura na hata baada ya kukamilika kwa mchakato wa uchaguzi Mkuu.

Mhe. Sendiga ametoa kauli hiyo leo Jumanne Oktoba 21, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari Mjini Babati kuhusu maandalizi mbalimbali ya kiserikali kuelekea uchaguzi Mkuu, akihimiza ushirikiano zaidi kati ya serikali, Wananchi, Vyama vya siasa na wadau wengine kuelekea kwenye uchaguzi huo Mkuu wa wiki ijayo Oktoba 29, 2025.


"Kama serikali tunawajibu wa kukemea mapema, yeyote ama kundi linalopanga kufanya vurugu kwa kujishawishi mwenyewe ama kushawishiwa kwa makusudi ama kwa bahati mbaya kwenda kutufanyia vurugu katika siku hii, sisi kama serikali tunatoa onyo kubwa na kali kabisa hatutokuacha salama na hatutakuvumilia. Amua mapema unakuja Mtaani tukutane ama tupige kura kwa amani turudi nyumbani.

"Hatutamvumilia atakayevuruga siku hii maalumu kwa upigaji wa kura. Mkoa wa Manyara ni "Wrong number",kamwe usijaribu kuvuruga siku hii ya neema na baraka kwa wananchi kuamua hatma ya miaka yao mitano ijayo." Amesema Mhe. Sendiga.

Mhe. Sendiga pia ametoa wito kwa wananchi wote wenye sifa kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kusisitiza umuhimu wa kurejea nyumbani na kuendelea na shughuli nyingine badala ya kuendelea kujihusisha na uvunjifu wa sheria ikiwemo kusalia vituoni kama ambavyo baadhi ya Vyama vya siasa vinavyoshawishi wanachama wao kusalia vituoni ili kulinda kura suala ambalo ni kinyume na miongozo ya uchaguzi Mkuu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI