Header Ads Widget

FISI WAUAWA BUSEGA, WAKUTWA NA SHANGA, HERENI NA ALAMA

 


Costantine Mathias, Busega-Simiyu.


FISI 17 wameuwawa katika oparesheni maalum ya kutokomeza wanyama hao katika Kata ya Shigala Wilaya ya Busega mkoani Simiyu, kufuatia kuwa tishio kwa maisha ya binadamu na mifugo.


Kufuatia oparesheni hiyo, kilichoshangaza wananchi wengi ni fisi wawili kati ya 17 waliouwa kukutwa na alama pajani, shanga shingoni na heleni sikioni.


Askari Mkuu wa Wanyamapori kutoka Pori la Akiba Kijereshi, Tuvako Michael, amewaka wananchi kutoka Kata jirani ikiwemo kabita kushirikiana katika oparesheni hiyo pamoja na kuchukua tahadhari dhidi ya wanyama hao.


Oparesheni hii imefanyika kwa siku saba, kufuatia hivi karibuni watoto wawili kushambuliwa na wanyama Fisi kwa nyakati tofauti katika Kijiji Cha Ihayabuyaga Kata ya Shigala, mmoja akiuwawa na mwingine kujeruhiwa.


Mwisho. 






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI