Header Ads Widget

EWURA YATOA WITO KWA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI KATIKA MATUMIZI YA GESI YA KUPIKIA


Na Samwel Mpogole - Mbeya

 Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kubwa wanapotumia gesi ya kupikia ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika, ikiwemo milipuko na moto.

Wito huo umetolewa na Bw. Francis Mhina, Afisa anayeshughulikia Malalamiko na Huduma kwa Wateja kutoka EWURA – Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja. Katika kuadhimisha wiki hiyo, EWURA imeweka kambi ya kutoa elimu kwa wananchi katika Stendi ya Mabasi ya Kabwe, jijini Mbeya, kwa lengo la kuwapa wananchi uelewa kuhusu matumizi salama ya nishati na maji pamoja na kusikiliza maoni yao.

“Ni muhimu wananchi wakatambua kuwa gesi ya kupikia ni salama iwapo itatumika kwa kufuata taratibu sahihi. Tumeendelea kushuhudia baadhi ya ajali zinazotokana na uzembe au kutozingatia kanuni za usalama, jambo ambalo linaweza kuepukika kabisa,” alisema Bw. Mhina.

Kwa upande wao, baadhi ya wananchi waliohudhuria na kupata Elimu hiyo akiwemo Bi. Magreth John na Bw. Adam Andason, wamesema wamefaidika kwa kiasi kikubwa na elimu waliyoipata, na wameiomba EWURA kuendelea kutoa elimu hiyo kwa maeneo mengine ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.

EWURA inaendelea na kampeni ya kutoa elimu kwa umma kuhusu haki na wajibu wa watumiaji wa huduma za nishati na maji, pamoja na kuhimiza matumizi salama ya huduma hizo, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa mwaka huu.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI