Na Mwandishi Wetu, Matukio Daima App Kisarawe
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Pwani Dk Dk Chakou Tindwa wagombea wa chama hicho wana uwezo mkubwa wa kuleta maendeleo.
Dk Tindwa ameyasema hayo Makurunge Kata ya Kiluvya Wilaya ya Kisarawe wakati wa kuhitimisha kampeni za Ubunge Jimbo la Kisarawe za Mgombea Dk Seleman Jafo.
Tindwa amesema kuwa ametembelea nchi mbalimbali za jirani na kuona kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo kwenye miundombinu ya barabara, umeme, maji, afya, elimu na huduma mbalimbali za kijamii
Amesema wananchi wa Kisarawe wahakikishe Oktoba 29 wanawachagua wagombea wa CCM Rais Dk Samia Suluhu Hassan, mbunge Dk Seleman Jafo na Diwani wa Kata hiyo Wakili Aidan Kitale.
Naye mwenyekiti wa kamati ya ushindi ya CCM kanda ya Mashariki Sophia Simba amesema kuwa kwa mara ya kwanza Tanzania inaweka historia kwa mgombea mwanamke kuwania Urais.
Kwa upande wake mgombea wa Ubunge Jimbo la Kisarawe Dk Seleman Jafo amesema kuwa endapo atachaguliwa atahakikisha kuwa vitongoji 79 vitapata huduma ya umeme, kusimamia miradi mikubwa ya maji ili maji yawe ya uhakika, ujenzi wa barabara, huduma za elimu na afya.





0 Comments