Na COSTANTINE MATHIAS, Bariadi.
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Bariadi Mjini kupitia CCM, Mhandisi Kundo Mathew amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi Oktoba 29, 2015, kumpiga kura Dk. Samia Suluhu Hassan sababu amedhamiria kumaliza kero za Wananchi ikiwemo tatizo la Umeme.
Akizungumza kwenye mikutano ya kampeni iliyofanyika katika Mitaa ya Bupandagila (kata ya Nyakabindi) na Mahaha (kata ya Bunamhala), amesema kuwa Mgombea Urais anatosha kuwatumikia wananchi kutokana na Mafanikio aliyoyaonyesha miaka minne iliyopita.
Amesema kuwa, Dk. Samia amedhamiria kuondoa changamoto ya nishati ya Umeme, wananchi wataongeza ajira na kukuza vipato vya familia kwa kufungua salooni na uchomeleaji.

"Kuanzia mwakani tutakuwa na uhakika wa Umeme baada gridi ya Taifa kukamilika Imalilo, Umeme utaiunua Uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla...Tunaenda kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya CCM ili wananchi wapate huduma za kijamii" Amesema Mhandisi Kundo.
Amesema kuwa serikali itakamilisha usambazaji wa Umeme kupitia Mradi wa Compact Mission 300 ambao utatekelezwa Mahususi kwa ajili ya kata za Mji wa Bariadi ili kuondokana na changamoto ya nguzo za Umeme na Mradi huo utafikisha huduma hiyo muhimu kwa Wananchi ili kuchochea ukuaji wa uchumi.

Mgombea Udiwani kata ya Nyakabindi kupitia CCM, Elias Masanja amewataka wananchi kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi pamoja na viongozi wake ili waendelee kuchapa kazi na kuwaletea Maendeleo.

Mgombea Udiwani kupitia CCM, kata ya Bunamhala Nkamba Zabron amewataka wananchi kumpigia kura za kishindo Dk. Samia Suluhu Hassna, Mgombea Ubunge Mhandisi Kundo Mathew pamoja na yeye (diwania) ili washirikiane kuwaletea Maendeleo.
Mwisho.
0 Comments